Wachezaji na makocha wa Chelsea walilazimika ‘kupiga’
miguu umbali mdogo kutoka uwanjani baada ya basi lililokuwa linawapeleka
uwanjani kukwama.
Basi hilo lilikwama katikati ya ukuta wakati
likipita kuingia uwanjani kabla ya kuwashusha wachezaji ili waingie vyumbani kwenye Uwanja huo tayari kuivaa PSG.
Juhudi za dereva kulikwamua zilishindikana kwa
zaidi ya dakika tano.
Kutokana na hali hiyo, Kocha Jose Mourinho
aliamuru wachezaji na wengine waliokuwa ndani ya basi kushuka na kutembea hadi
vyumbani.
Katika mechi hiyo jijini Paris, Chelsea waliokuwa wageni walipata sare
ya bao 1-1.











0 COMMENTS:
Post a Comment