WACHEZAJI WA YANGA WAKIWA KATIKA UWANJA WA LOBATSE, BOTSWANA. |
Yanga imeonyesha haitaki utani baada ya kumtimua Ofisa wa Jeshi la
Botswana (BDF) mwenye cheo cha luteni ambaye alikuwa amefika katika Hoteli ya
Oasis nje kidogo ya Jiji la Gaborone, Botswana.
Yanga wako jijini hapa kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya Kombe
la Shirikisho dhidi ya BDF XI itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Lobatse.
MRISHO NGASSA NA SIMON MSUVA WAKILAMBA INTERVIEW YA CLOUDS TV WAKIWA KWENYE UWANJA WA LOBATSE NCHINI BOTSWANA AMBAKO LEO WANAKIPIGA HAPO. |
Aliyeanzisha kasheshe hilo ni Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas
Tiboroha ambaye alimtaka ofisa huyo wa jeshi kuondoka mara moja kambini hapo.
Hali hiyo ilionyesha kumuudhi sana ofisa huyo ambaye alilaumu
kutokana na tukio hilo na kusisitiza kwamba katibu huyo hakuwa mwanamichezo,
lakini Dk Tiboroha hakutaka kulizungumzia zaidi ya kusisitiza usalama wa kikosi
chake ndiyo jambo muhimu.
“Ni kweli katibu amemtaka ofisa huyo aondoke katika eneo la hoteli.
Unajua jana (juzi) walikuja hapa hotelini maofisa watatu, waliungana na sisi
baada ya kuikataa Hoteli ya Grande,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari cha
Yanga, Jerry Muro na kuongeza:
“Sasa leo (jana) asubuhi amekuja mwingine mmoja ambaye alifika
mapema hata kabla hatujaanza kunywa chai. Katibu akaona hilo siyo sawa,
ukizingatia huyo ni mwanajeshi, akamfuata na kumueleza aondoke.
“Jamaa alichukia, ila nimekaa naye tena na kumuelezea kuwa hapa hotelini
tunamhitaji mtu mmoja tu kutoka BDF. Sisi pia tulifanya hivyo na hakuna
kiongozi wetu aliyekwenda kambini kwao walipokuwa Dar.”
0 COMMENTS:
Post a Comment