Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe licha ya kuwa gumzo kubwa baada
ya kufunga mabao mawili dhidi ya BDF XI bado anaendelea kuwa na rekodi ya
mchezaji pekee wa Yanga anayeujua vizuri Uwanja wa Lobatse utakaotumika kwa
mechi ya leo.
BDF inaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Lobatse ulio kilomita 70
kutoka jijini hapa na Tambwe atacheza kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo
miezi kadhaa iliyopita wakati timu yake ya taifa ya Burundi kulala kwa bao 1-0
na kung’olewa katika kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Mechi hiyo kuwania kucheza Afcon ilipigwa Juni Mosi, 2014 na Burundi
ikalala kwa bao hilo huku Tambwe akishindwa kutikisa nyavu za Waswana hao.
Julai Mosi, 2014, Botswana ikacheza mechi kirafiki dhidi ya Tanzania
na kuichapa mabao 4-2, safari hii mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Taifa
ulio hapa katika Jiji la Gaborone.
Kwa Tambwe, itakuwa ni mara ya nne kukutana na timu za Botswana
ndani ya miezi saba. Mara ya kwanza walipotoka sare ya bila kufungana mjini
Bujumbura, halafu wakalala kwa bao 1-0 huko Lobatse.
Mara ya tatu ni jijini Dar, safari hii akiichezea Yanga na
kufanikiwa kufunga mabao yote katika ushindi wa 2-0. Swali, leo ataendelea
kuonyesha sasa anawajulia Waswana?
0 COMMENTS:
Post a Comment