RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA AKIZUNGUMZA MBELE YA MAKAMU WAKE, KABURU (KUSHOTO) WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI NA WANACHAMA WA KLABU HIYO, LEO. |
Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' wamewaambia wanachama wao kuwa hawana tofauti.
MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA, KABURU AKITAFAKARI. |
Kumekuwa na taarifa za Kaburu kutuhumiwa na wenzake kwamba anaihujumu timu, lakini Kaburu amekuwa akikanusha hilo.
Katika kikao cha wanachama kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Osyterbay jijini Dar, wawili hao walikanisha kabisa suala hilo.
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI, MUSLEY AL RAWAH NA SAID TULLY |
Kaburu alisisitiza wamekuwa wakishirikiana vizuri na Aveva ambaye amekuwa kiongozi wake hata kabla ya kukutana katika urais na makamu.
Hata hivyo, viongozi hao hawakuweka wazi bayana kama kuna matatizo ndani ya klabu hiyo na hasa baadhi ya viongozi kutoelewana.
Baadhi ya wanachama walikuwa wakitaba Kaburu kuondolewa kwa madai wamekuwa wakisikia kwamba anaihujumu timu, jambo ambalo ameendelea kulikanusha.
Wanachama wa Simba walijitokeza 'kinyonge', yaani idadi ndogo hata kuliko ilivyotarajiwa.
Baada ya mkutano huo, baadhi ya wanachama walisisitiza kwamba wanajua kuna tatizo kati ya viongozi wao, lakini hawakutaka kuweka bayana.
Hivyo wakasisitiza, viongozi kumaliza tofauti zao ili kuisaidia klabu yao kubadilika na kuwa na kikosi chenye uwezo wa kupambana.
0 COMMENTS:
Post a Comment