Rais wa Simba, Evans Aveva, ametoa maagizo mazito kwa
benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Mserbia, Goran Kopunovic
kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyo mbele yao.
Mabingwa hao wa zamani wa Bara, wamebakiwa na michezo
saba kabla ya kumaliza msimu huu ambayo ni sawa na dakika 630.
Simba ipo nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu kwa kuwa
na pointi 29 nyuma ya Azam yenye pointi 33 na Yanga yenye 34.
Aveva amesema kuwa
moja ya mikakati waliyojiwekea ni kuhakikisha wanashinda michezo yote
iliyobakia kwa kutoa maagizo katika benchi la ufundi kuhakikisha agizo hilo
linatekelezeka.
“Kwa sasa hatutazami suala la ubingwa wa ligi msimu huu
ila tunachotaka ni kuweza kushinda michezo yetu yote iliyobakia na tayari
nimeshatoa maagizo katika benchi la ufundi kwa ajili ya utekelezaji.
“Tunahitaji kumaliza katika nafasi nzuri, hivyo ni
lazima tufanye vyema katika mechi zilizobakia bila kupoteza,” alisema Aveva.







0 COMMENTS:
Post a Comment