Hans Mloli na Sweetbert Lukonge
KIKOSI cha Azam kimetua nchini jana
mchana kikitokea Sudan baada ya kutupwa nje ya El Merreikh ya Sudan kwa jumla
ya mabao 3-2, lakini wachezaji wa timu hiyo wamemshutumu vikali mwamuzi kwamba
aliwaua waziwazi.
Azam walijikuta wakifungwa mabao 3-0,
mawili yakiwa katika dakika tano za mwisho. Awali walikuwa wameshinda 2-0
jijini Dar es Salaam, hivyo walitarajiwa waongeze umakini kulinda mabao yao
ugenini.
Championi lilizungumza na wachezaji
wawili wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo, Mrundi, Didier Kavumbagu na Erasto
Nyoni muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) na kuweka wazi kilichotokea kwenye mechi hiyo na kuelezea
masikitiko yao.
Kwa upande wa Erasto alielezea hivi:
“Mabao waliyotufunga yalikuwa ya halali tu lakini ishu ilikuwa wanabebwa kwenye
baadhi ya matukio muhimu uwanjani, yaani muda mwingine refa anawabeba bila
sababu, tukitaka kwenda kufunga wanasema offside wakati muda mwingine ni uongo
tu.
“Watanzania tunacheza mpira sana ila
tukifika ugenini ndiyo tatizo linapokuwepo yaani kunakuwa na mambo ya
ajabuajabu mpaka inafikia hatua hii, ifike hatua na sisi tubadilike na sisi
wakija huku iwe ni fitna tu na si ‘fair play’ ndiyo tutafika mbali.”
Kavumbagu naye kwa upande wake
akafunguka: “Yaani hakukuwa na fair yoyote ile, refa alionyesha dhahiri kwamba
nia yake ni ipi tangu mwanzo wa mechi mpaka mwisho, kuna kipindi tunaenda
kufunga, anasema kwamba ni offside, tunachezewa rafu yeye anapeta tu, ila
wakiguswa El Merreikh anapiga filimbi.
“Kuna wakati nilichezewa rafu,
akapeta, nikamuuliza refa mbona unapeta tu, tatizo nini, akanitukana (tusi
halifai kuandikika gazetini), yaani tangu nianze kucheza mpira sijawahi
kutukanwa na refa, ndiyo kwanza imenitokea Sudan.
“Halafu wakati tupo mapumziko kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo, kocha Omog (Joseph raia wa Cameroon) alimsikia kocha
msaidizi wa Merreikh anamwambia kwa Kifaransa huyo refa ambaye ni Mzambia kuwa
tulielewana mpaka mapumziko tuwe na mabao mawili mbona mpaka sasa moja? Wakawa
wanabishana pale.”
0 COMMENTS:
Post a Comment