March 2, 2015




Na Louis Ngwako, Gaborone
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameelezwa ndiyo kikwazo kikubwa cha BDF XI kushindwa kupata bao la tatu ikiwa ugenini.

Mshambuliaji hatari wa BDF, Kumbulani Madziba ambaye aliifunga Yanga bao moja kati ya mawili wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwao katika mechi ya Kombe la Shirikisho, amesema Cannavaro ndiye alikuwa kizingiti kikubwa.


Akizungumza mjini hapa, Madziba alisema walikuwa na nafasi ya kufunga mabao ya vichwa, lakini Cannavaro hakuruhusu wapige mipira ya vichwa.

“Karibu asilimia tisini ya mipira yote ya vichwa langoni mwao alipiga yeye. Tulijaribu kubadilisha hata upigaji wa krosi, ziende nyuma ya lango, lakini aliiwahi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic