Timu
ya taifa ya soka la ufukweni ya Oman ndiyo mabingwa wa Asia na sasa watashiriki
michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Ureno.
Kazi
yote ni sifa zimuendee kocha wao mkuu, Talib Hilal ambaye ni beki wa zamani wa
Simba.
TALIB AKITOA MAELEKEZO KWA KIKOSI CHAKE AMBACHO SASA NDIYO MABINGWA WA BARA LA ASIA NA WAWAKILISHI KATI YA WATATU WA BARA HILO KATIKA KOMBE LA DUNIA LITAKALOPIGWA NCHINI URENO. |
Hilal
ameipeleka timu hiyo fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi mfululizo katika michuano ya Asia huku fainali
wakiwatwanga Japap mabao 3-2 kwa mikwaju ya penalti.
Usisahau pamoja na Hilal, kocha msaidizi wa kikosi hicho ni Mtanzania, Yusuf Abeid, kipa wa zamani wa Pamba ya Mwanza.
Usisahau pamoja na Hilal, kocha msaidizi wa kikosi hicho ni Mtanzania, Yusuf Abeid, kipa wa zamani wa Pamba ya Mwanza.
Lakini
kabla ya hapo walikuwa wamejihakikishia kucheza Kombe la Dunia baada ya
kuwafunga Lebanon kwa mabao 5-4.
Kabla
ya hapo, hatua ya robo fainali, Oman ya Talib walionyesha kweli wanajua baada
ya kuwakung’uta China kwa mabao 7-2.
Michuano
hiyo ya Asia iliunguruma jijini Doha, Qatar kuanzia Machi 23 hadi 28 na Oman
ndiyo wababe zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment