Louis
van Gaal ameibuka mshinda wa tuzo maarufu ya Anton Geesink.
Tuzo
hiyo maalum hutolewa nchini kwao Uholanzi kwa mtu, mji au kundi la watu
lililofanya vema katika michezo.
Van
Gaal ambaye amekuwa akihaha na kikosi chake cha Man United, amepewa tuzo hiyo
baada ya Uholanzi kuonyesha kiwango bora na kushika nafasi ya tatu katika Kombe
la Dunia nchini Brazil, mwaka jana.
Mambo
yamekuwa si mazuri sana kwake akiwa na Man United, lakini sasa angalau iko
katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England na wikiendi hii ina
kibarua kigumu dhidi ya Aston Villa.
0 COMMENTS:
Post a Comment