Kipa bora msimu uliopita,
Hussein Shariff ‘Casillas’ wa Simba, amewatolea uvivu mashabiki wa timu hiyo
kuwa wamtarajie baada ya miezi mitatu, sawa na siku 90 ambapo atakuwa tayari
kupigania namba tena mbele ya Ivo Mapunda.
Kipa huyo wa zamani wa
Mtibwa Sugar, ndiye anamiliki tuzo ya kipa bora msimu uliopita, lakini amekuwa
na wakati mgumu Simba kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambapo hajaonekana
dimbani tangu kuanza kwa mwaka huu.
Casillas alisema licha ya
kurejea kwa muda mrefu lakini bado anajisikia hajawa katika kiwango cha
kupigania nafasi mbele ya Ivo.
“Sijawa fiti, siwezi
kuongopea mashabiki kwamba nimepona. Ninavyojisikia nahitaji miezi kama miwili,
mitatu ndipo nitarejea kupigania nafasi kikosi cha kwanza, lakini kwa sasa
najifua zaidi,” alisema Casillas.
Simba imekuwa ikiwategemea
mkongwe Mapunda pamoja na kinda Peter Manyika ambaye amekuwa chaguo la pili
tangu kuumia kwa Casillas.
0 COMMENTS:
Post a Comment