Baadhi ya viongozi wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), juzi Jumamosi walijikuta wakitofautiana
baada ya mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, kuifungia timu yake hiyo
bao la ushindi katika dakika za majeruhi ilipopambana na Mtibwa Sugar kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao hilo liliiwezesha Simba
kubakiza pointi mbili tu ili kuifikia Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu
Bara.
Katika hali ya kushangaza,
baadhi ya wajumbe wa TFF, waliokuwa katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo
uliofanyika juzi Jumamosi na jana Jumapili, walipagawa kwa furaha baada ya
kupata taarifa za bao hilo la Okwi huku wengine waliokuwa ni wa Yanga kuonekana
wakiishiwa pozi.
Bila ya woga wowote, wajumbe
wanazi wa Simba walianza kupongezana huku wakipeana mikono na kukumbatiana na
viongozi wa Simba, rais wa klabu hiyo, Evans Aveva pamoja na makamu wake,
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambao pia walikuwa mjini hapa kwa ajili ya mkutano huo.
“Tulikuwa tunawapongeza
viongozi hao kwa kupata matokeo mazuri ya ushindi katika mechi zao tatu
mfululizo tena dhidi ya timu kubwa.
“Lakini pia kitendo cha
kumsajili Okwi kinaonekana kuwa kilikuwa na maana kubwa kwao kwani faida yake
imeanza kuonekana, hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya sisi kuwapongeza viongozi
hao,” alisema Jackson Songora, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza
(MZFA) huku akiungwa mkono na wajumbe wengine ambao pia walionekana kufurahishwa
na matokeo hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment