Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), limeombwa kuacha mara moja kuingilia kazi za Bodi ya Ligi na kuzitaka
pande zote mbili kufanya kazi kiweledi.
Rai hiyo lilitolewa jana na
wajumbe 250 kwenye Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika katika Hoteli ya Morogoro,
mkoani Morogoro kwa siku mbili.
Hivi karibuni kumekuwepo na
mkanganyiko wa TFF kutajwa kuingilia kazi za Bodi ya Ligi, ikiwemo kupanga
ratiba.
Wakizungumza kwenye kilele
cha mkutano huo, wajumbe walisema mambo yameonekana kutoenda sawa kwenye Bodi
ya Ligi na hiyo imetokana na muingiliano wa kikazi na TFF.
“Tunawaomba TFF na Bodi ya
Ligi, muwe na mipaka katika utendaji wenu, TFF muache kuingilia kazi na maamuzi
ya Bodi ya Ligi. Ndiyo maana kumekuwepo na changamoto nyingi sana,” alisema mmoja
wa wajumbe wa mkutano huo.
Kwa upande wa TFF, wamesema
watalifanyia kazi suala hilo na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano
na bodi na siyo kuingilia kazi zao.
0 COMMENTS:
Post a Comment