Pamoja na Mrisho Ngassa kusema huu ndiyo msimu
wake wa mwisho kuichezea Yanga, uongozi wa timu hiyo umesema hauna mpango wa
kuachana na winga huyo na utahakikisha anabaki katika kikosi chao.
Mapema wiki hii, Ngassa amenukuliwa akisema mwishoni mwa msimu ndiyo mwisho wake Yanga na sasa anatakiwa na timu zikiwemo za Afrika Kusini, DR Congo na Qatar.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa
Yanga, Jerry Muro, amesema: “Msione tupo kimya licha ya
Ngassa kutamka vitu vingi, bado tuna mpango wa kukaa naye meza moja ili
kujadili mkataba mpya.
“Hatujakata tamaa ya kumbakiza kwa kauli
alizotoa za kutaka kuondoka, lengo letu tuwe naye kwani ana mchango mkubwa
kwenye timu.”
Mkataba wa Ngassa na Yanga unaisha mwisho wa
msimu huu wa Ligi Kuu Bara lakini amekuwa hana furaha na klabu hiyo kutokana na
deni la Sh milioni 45 analodaiwa na benki moja ambalo anadai klabu yake
imekiuka makubaliano ya kumlipia.
0 COMMENTS:
Post a Comment