Timu ya Kiluvya United ya mkoa
wa Pwani jana imetawazwa Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya
kuifunga Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika
kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
Kiluvya United inaunganana
timu za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma, Mbao FC ya Mwanza na Mji Njombe ya Njombe
kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL)msimu ujao, huku timu za Ujenzi Rukwa,
Katavi FC na Volcano zikishuka daraja kutoka Ligi Daraja la Pili.








0 COMMENTS:
Post a Comment