Yanga itaendelea
kukosa huduma ya kiungo wake mwenye kasi Mrisho Ngassa.
Ngassa amefanya
mazoezi leo asubuhi na kikosi hicho, lakini bado anaonekana kutokuwa fiti.
Hivyo ataukosa
mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu JKT kama alivyouokosa uliopita dhidi ya Mgambo
Shooting mjini Tanga.
Ngassa aliuokosa
mchezo huo kwenye Uwanja wa Mkwakwani huku Yanga ikishinda kwa mabao 2-0.
Hata hivyo,
ilionekana wazi alikuwa akihitajika hasa kupitia kasi yake kubwa.
Ngassa amekuwa
akilishirikiana na Simon Msuva kupandisha kasi ya mashambulizi ya Yanga na
huenda akakaa nje kwa zaidi ya siku nyingine tatu zijazo.







0 COMMENTS:
Post a Comment