Msafara wa watu 25 wa timu ya
Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya
alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza
tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya
jumapili.
Katika msafara huo utakaokuwa na
wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi
amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa
katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wanaocheza soka la
kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black
Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of
Pretoria).
Wengine ni Nahodha Joseph
Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR), Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango
Kayira (Costal De Sol - Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).








0 COMMENTS:
Post a Comment