Mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye
anakipiga Yanga kwa sasa, Danny Mrwanda, amewaomba radhi mashabiki na wachezaji
wa Simba kufuatia adhabu aliyopigwa na TFF kwa kukataa kupeana mikono na
wachezaji wa Simba.
Mrwanda aliyewahi kukipiga Long DT ya Vietnam amepigwa faini ya laki tano
kufuatia kitendo cha ‘kukwepa’ kupeana mikono na wachezaji wa timu pinzani
kabla ya mchezo wakati timu hizo zilipokutana Machi 8, mwaka huu na Simba
kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kanuni zinaeleza ni lazima wachezaji
wapeane mikono pamoja na marefarii.
Mrwanda amesema watu wa Simba wasimfikirie kivingine, kwani hakudhamiria, bali
alikwenda kunywa maji kabla ya kuanza kwa pambano lakini siyo kuwakwepa.
“Nilishangaa kusikia nimepigwa faini,
lakini naomba wasinielewe vibaya, sikudhamiria kuwakimbia, nilikwenda kunywa
maji na kocha akawa ananipa maelekezo, niliporudi nikakuta wamemaliza, lakisi
siyo kusema niliwakimbia.
“Sikujua kama ni kosa na utaona
nilipeana na baadhi yao baadaye. Sina kinyongo na mchezaji yeyote Simba jamani.
Ila yote kwa yote nitakubali kulipa maana ni maamuzi yao (TFF) wakubwa,”
alisema straika huyo wa zamani wa Polisi Moro.
0 COMMENTS:
Post a Comment