Klabu ya Simba imeanza mazungumzo na
baadhi ya wachezaji wake kwa ajili ya kuwaongezea mikataba mipya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema wameanza mazungumzo na wachezaji hao ili
kuhakikisha waliopanga kuwabakiza wanabaki.
“Kuna wachezaji watatu kati ya hao
ambao tumeshaanza nao mazungumzo ambao ni Ivo, Baba Ubaya na Singano. Hao
wengine tutakuwa na kikao wiki ijayo (wiki hii) kwa ajili ya kuwajadili,”
alisema Hans Poppe.
Baada ya kumalizana na hao watatu,
Simba itaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji wengine kwa ajili ya
kuwaongezea mikataba.
0 COMMENTS:
Post a Comment