Kiungo mshambuliaji wa Yanga,
Mbrazili, Andrey Coutinho, ambaye hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu, leo
Jumatatu anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi kutokana na hali yake kuendelea
kuimarika.
Coutinho amekaa nje ya uwanja kwa
wiki tano akiuguza goti. Aliumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City
Februari 24, mwaka huu ambapo Yanga ilishinda 3-1.
Coutinho amesema kuwa anamshukuru Mungu kwani hali yake inaendelea vizuri.
“Ninamshukuru Mungu kwani hali yangu
inaendelea vizuri na inaleta matumaini, hivyo kesho Jumatatu ninaanza mazoezi
mepesi kutokana na ripoti ya daktari wangu,” alisema.
Alipomtafutwa daktari wa
Yanga, Juma Sufiani, ili kuhakikisha taarifa hizo alisema: “Ni kweli Coutinho
anaendelea vizuri ambapo kesho (leo) nimemruhusu aanze mazoezi mepesi ili
kuimarisha zaidi viungo vyake.”
0 COMMENTS:
Post a Comment