![]() |
| CRYUFF (KUSHOTO)... |
Kocha wa zamani wa
Barcelona na gwiji wa klabu hiyo, Johan Cruyff amesema hakufurahishwa na mchezo
uwezo waliouonyesha Barcelona.
Cruyff raia wa
Uholanzi ambaye alikuwa mchambuzi wakati wa mchezo huo, amesema hakufurahishwa
na kiwango walichokionyesha Barcelona.
Hata hivyo
alisisitiza, alifurahia ushindi wa mabao 2-1 kwa kuwa timu yake ndiyo
iliyoibuka na ushindi.
“Si vibaya kufurahia
ushindi wakati hamkuonyesha kiwango bora, lakini siwezi kusema ulikuwa ushindi
bora,” alisema.
Barcelona
ilifanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani dhidi ya Real Madrid, hata
hivyo haikuonyesha kiwango cha juu sana kama ilivyokuwa imetazamiwa.









0 COMMENTS:
Post a Comment