Yanga inashuka
dimbani kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tayari kumenyana na
JKT Ruvu ili kusaka pointi tatu muhimu.
Kocha Mkuu wa Yanga,
Hans van der Pluijm amesema pointi hizo tatu ni kuhimu kwa kuwa ndiyo watakuwa
timu ya kwanza kufikisha pointi 40.
“Kushinda kila mechi
ni muhimu, lakini mechi hii inaweza kuwa ni muhimu zaidi.
“Tukifikisha pointi
arobaini litakuwa moja ya jambo muhimu katika kipindi hiki. Lazima tushinde na
wachezaji wanalijua hilo.
“Tunajua hatuwezi
kushinda kilahisi kwa kuwa ligi ni ngumu na kila timu ina kiwango bora,”
alisema Pluijm.
Azam FC ndiyo
inayoipa Yanga presha ya juu zaidi kwa kuwa ina pointi 36 ikiwa ni tofauti ya
pointi moja tu.
Mabingwa hao
watetezi nao wamekuwa na mwendo mzuri wa ushindi, hali inayoilazimu Yanga
kuhakikisha haitelezi.







0 COMMENTS:
Post a Comment