Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm
amesema watacheza soka la kushambulia zaidi katika mechi yao dhidi ya Simba,
leo na wana nafasi ya kufunga mabao manne katika mechi hiyo.
Yanga na Simba zinakutana leo kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara.
Lakini akasisitiza kuwa amezungumza na
wachezaji wake na kuwasisitiza suala la kuzitumia nafasi wanazozipata.
“Tunaongoza kwa kutengeneza nafasi, lakini
hatuzitumii. Wachezaji wanalijua hilo, hivyo ni lazima tufunge.
“Tima uwezo wa kufunga mabao mawili kila
kipindi. Hilo ndiyo lengo lakini lazima tuwe makini na kuwekeza akili katika umaliziaji
hasa kwa washambuliaji,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment