Dunia ina mambo! Ule uwanja wa Mane Garrincha sasa
unatumika kama sehemu ya madereva kubadilisha mabasi.
Mabasi ya abiria ya serikali zaidi ya 300
yamekuwa yakikutana kila siku kwenye uwanja huo kwa ajili ya madereva
kubadilisha shifti.
Gazeti la The Mirror la Uingereza limesema
uwanja huo wa pili kwa kuwa ghali zaidi katika historia ya soka duniani, sasa
unatumika kwa kazi hiyo ambayo si yake.
WAKATI WA KOMBE LE DUNIA. |
Serikali ya Brazil ilimwaga pauni milioni 350
kuutengeneza uwanja huo kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka jana na una uwezo wa
kuingiza mashabiki 72,000 wakiwa wameketi.
Ndiyo uwanja ghali zaidi ukiwa wa pili baada ya
Wembley wa Uingereza.
0 COMMENTS:
Post a Comment