Klabu ya Sunderland ya
England imetangaza kumtimua kocha wake Gus Poyet raia wa Uruguay.
Poyet ameifundisha
Sunderland kwa siku 525 tokea Oktoba 8, 2013.
Kocha huyo amefukuzwa baada
ya kuchapwa mabao 4-0 na Aston Villa licha ya kuwa nyumbani.
Aliingoza timu hiyo katika
mechi 75, akashinda mechi 23, akapoteza 22
na sare 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment