Timu ya soka ya taifa,Taifa
Stars imewasili salama leo asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya
mchezo wa kirafiki wa Kimataifa siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu
ya Taifa ya Malawi, The Flames, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba.
Kikosi cha Stars kimeondoka
kikiwa na wachezaji 18 ambao wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji
Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na
wenzake leo mchana jijini Mwanza.
Wachezaji waliopo kambini jijini
Mwanza ni, magolikipa Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto
Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar),
Haji Mwinyi (KMKM), Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
Wengine ni Amri Kiemba, Frank
Domayo, Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo
(Stand United), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC
amejiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans
wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo
wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya Jumatano.







0 COMMENTS:
Post a Comment