TALIB (WA PILI KUSHOTO) NA ABEID (ANAYEMFUATIA) WAKISHEREKEA BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA GHUBA JIJINI DOHA, QATAR, JANA. |
Oman
imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ghuba kwa upande wa soka la ufukweni.
Oman
inayofundishwa na beki wa zamani wa Simba, Talib Hila na kipa wa zamani wa
Pamba, Yusuf Abeid imeshinda mechi zake zote tano.
Oman
ambao kwa sasa ndiyo mabingwa wa dunia walianza kwa kuwachapa Bahrain kwa mabao
4-3, halafu wakawapa kipigo wenyeji Qatar 4-1.
Kama
hiyo haitoshi wakawachapa Kuwaiti kwa mabao 4-2 kabla ya kuishushia kipigo UAE
cha mabao 5-3.
Hivi
karibuni Talib na mwenzake Abeid, waliingoza Oman kubeba ubingwa wa dunia pia
kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Ureno.
Timu
ya taifa ya Oman ya soka la ufukweni inaonekana kuwa tishio kwa upande wa bara
la Asia.
0 COMMENTS:
Post a Comment