WACHEZAJI WA ETOILE DU SAHEL WAKIJIFUA VILIVYO KABLA YA MECHI KADHAA ZA LIGI KUU YA TUNISIA PAMOJA MECHI YA KOMBE LA SHIRIKISHO DHIDI YA YANGA. |
Imevuka kwa kuzifunga
timu za BDF ya Botswana na baadaye FC Platnum ya Zimbabwe.
Hauwezi ukasema Yanga
ilizitoa timu nyanya sana kwa kuwa tuliona namna zilivyocheza. Huenda kikosi
cha Yanga kilikuwa katika ubora sahihi.
Bado Yanga haijafika
katika safari iliyokuwa inahitaji kufika, vita iko mbele na inabidi kupambana
zaidi ya ilipo.
Sasa inakutana na
Etoile du Sahel ya Tunisia, timu ambayo ina kumbukumbu ya kung’olewa na Simba
katika michuano ya kimataifa.
Lazima inajua
machungu au ugumu wa timu za Tanzania na inajua kuwa Yanga ni moja ya klabu
kongwe barani Afrika.
Kamwe haiwezi kufanya
utani, ndiyo maana ukifuatilia, wameanza mazoezi mapema, wanapambana vilivyo na
wamepania kushinda.
Yanga hawapaswi kulala
kwa kufurahishwa na matokeo ya mechi zao nne za Kombe la Shirikisho dhidi ya
BDF XI na FC Platnum.
Lakini bado
hawatakiwi kusinzia na kuridhishwa na matokeo yao dhidi ya timu za Tanzania
Bara ambako imefikia hadi kuzikaanga timu kongwe kama Coastal Union kwa mabao
8-0.
Kikosi cha Yanga kina
mwelekeo mzuri wa kuwa imara, lakini bado hakijasimama katika hali ya kuwa
tishio sana hadi kwa timu kama Etoile.
Lakini ilipofikia
pia, haiwezi kuwa timu dhaifu ya kuihofia Etoile hadi watu wachanganyikiwe. Kikubwa
ni umakini, malengo na viongozi watambue wanakutana na timu ya namna gani na
nini cha kufanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment