April 11, 2015

BIN SLUM (WA PILI KUSHOTO) NA WADAU WENGINE WA COASTAL UNION WAKISHEREKEA USHINDI WA COASTAL UNION, LEO. 
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ni faraja kubwa kwa Coastal Union.


KWani pamoja na kupoza machungu ya kufungwa mabao 8-0 dhidi ya Yanga, inasherekea kurejea kwa aliyekuwa mdhamini wake nassor Bin Slum ambaye ameongoza jahazi.

Bin Slum amesema kweli amerejea Coastal Union na kuzika tofauti zilizojitokeza.

“Pamoja na migogoro yote iliyopita, nimekuwa nikisisitiza mimi ni Coastal Union na siwezi kubadilika.

“Nina faraja pia, nimerudi na ushindi wa mabao hayo mawili na sasa ni kujitahidi kwa kushirikiana na wenzangu ili Coastal Union isiteremke daraja,” alisema akionekana ni mwenye furaha.

Mabao ya Coastal Union katika mechi hiyo yalifungwa na Mkenya Rama Salim na Mnigeria, Bright Obinna.

Ushindi huo unaifanya Coastal kufikisha pointi 27 na kuondoka kwenye timu zinazokwepa kuteremka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic