Baada ya Simba kupoteza mchezo wa juzi Jumamosi dhidi ya Mbeya City kwa mabao 2-0,
kipa wa timu hiyo, Peter Manyika, ameomba kuachwa kwa kile kinachodaiwa kushuka
kiwango chake kwa sababu ya mrembo anayefahamika kwa jina la Nima.
Simba
ambayo inaisaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ili msimu ujao iweze
kushiriki michuano ya kimataifa, inaonekana kuanza kuikosa kwani kwa sasa
inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 huku Azam wanaoshika nafasi ya pili
wakiwa na pointi 42.
Manyika
ambaye alidaka katika mchezo huo wa juzi, amechukizwa na matokeo hayo na kuamua
kufunguka kwa kuandika ujumbe uliokwenda sambamba na picha ya mrembo huyo
katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram akiomba kuachwa, ikiwa
uongozi wa timu yake unahisi hafanyi vizuri katika kikosi hicho.
Ujumbe
huo ulisomeka hivi: “Anayesema (mrembo) ananiua kiwango aje kudaka yeye sababu
mimi siyo (tusi), nina haki ya kuwa na mpenzi kama watu wengine, mkihisi
sifanyi kazi yenu mniache.”
Awali alipotafutwa kipa huyo na
kusema kwamba hataki kusema chochote kuhusu hilo kwa sababu ameamua
kuishi maisha yake binafsi, ndiyo maana amekuwa hafuatiliwi na watu.
Alipotafutwa
baba yake kipa wa zamani wa Yanga, Manyika Peter ambaye alifunguka: “Unajua
hiyo ishu bado sijaiona kwa sababu siku hizi nimekuwa sitembelei sana kwenye
mitandao, lakini mimi kwake ni kama mshauri, hivyo ni vyema uongozi wa Simba
uwe unakaa na wachezaji vijana kuwashauri mambo mbalimbali ambayo yatakuwa ni
muongozo mzuri katika maisha yao.”








0 COMMENTS:
Post a Comment