Mvua imeendelea kuwa tatizo
kubwa katika programu za Kocha Goran Kopunovic wa Simba.
Kopunovic amekiongoza
kikosi cha Simba kufanya mazoezi mepesi leo kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM).
Baada ya kupasha misuri na
kukimbia kwa kasi mwendo mfupi, baadaye wachezaji hao walinyoosha mwili na
kucheza “hangaisha bwege”.
Kopunovic alisema
walishindwa kuendelea zaidi kwa kuwa hawakuwa na nafasi kufanya mazoezi mazuri
kwa kuwa uwanja ulijaa tope.
“Hakuna ujanja, utaona
uwanja ulivyo mbaya kwa sasa. Hatuwezi kushindana na halisi,” alisema.
Hata jana, mambo yalikuwa
hayohayo baada ya Simba kushindwa kufanya mazoezi alichotaka kocha huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment