Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm
ameonya kuwa si sahihi kwa wachezaji wake kuungana kwenye sherehe za ubingwa
kabla ya kuishinda Polisi Moro, leo.
Yanga inaikaribisha Polisi Moro katika mechi
ya Ligi Kuu Bara, iwapo itashinda, basi itakuwa imejihakikishia kutwaa ubingwa
wa Tanzania Bara unaoshikiliwa na Azam FC.
Pluijm amesema mashabiki wana kila sababu ya
kuanza sherehe kwa kuwa ni furaha ya. Lakini wachezaji wana deni kubwa la
kuhakikisha wanatimiza ndoto yao.
“Mechi haitakuwa lahisi kwa kuwa Polisi wako
mkiani, sisi tuko kileleni. Kila mmoja ana vita yake, anataka kushinda.
“Kazi yetu ni kucheza na kuhakikisha tunafanya
vizuri, nimezungumza na wachezaji na nitaendelea kusisitiza kabla ya mechi,” alisema.
Yanga imekaa kileleni ikiwa na pointi 52,
ikishinda leo itafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC ambayo
ikishinda mechi zake zote tatu itakuwa na pointi 54.
0 COMMENTS:
Post a Comment