April 26, 2015

KAHABUKA AKIWANIA MPIRA NA KIJANA WA TIMU YA VIKAWE...
Makipa Juma Kaseja na Shabani Kado wameonyesha uwezo kwa kuwabeba Mavetarani wa Dar es Salaam waliosafiri hadi Vikawe, Bagamoyo kucheza mechi ya kirafiki iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.

SALEH ALLY AKIPAMBANA....

Mavetarani hao wakiongozwa na nyota wa zamani wakiwemo wanaong'ara sasa, walicheza mechi hiyo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe na kufanikiwa kuibuka na mabao 2-1.
MAKEKE YA MBWIGA...

Kaseja ndiye alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti kabla ya Kado kufunga la pili kwa shuti akiunganisha pasi nzuri ya Haruna Moshi 'Boban'.

Wenyeji waliokuwa na timu ya vijana tupu tena wenye kasi ya kimondo walitangulia kupata bao mwanzoni mwa kipindi cha pili huku Saleh Ally 'Jembe', Clement Kahabuka, Mbwiga Mbwiguke na Shaffih Dauda wakishindwa kusawazisha.

Baada ya bao hilo, wenyeji waliendelea kuisumbua ngome iliyokuwa ikiongozwa na George Masatu na Kamba Lufo.

Kuingia kwa Athumani Tippo, Kaseja na Boban, kulisaidia kugeuza sura ya mchezo na kufanya mambo yaende tofauti kwa maveterani hao kuanza kushambulia kwa kasi hadi walipofanikiwa kupata mabao hayo.

Wenyeji walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu, lakini soka safi la wageni liliwalazimisha kuanza kuwashangilia huku wengi wakivutiwa na Tippo ambaye pamoja na kuwa na umbo kubwa lakini alicheza kwa kujiamini na kuwapa shida vijana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic