Kamati ya Rufaa ya Nidhamu (TFF) imekutana leo tarehe 12/04/2015
kujadili rufaa No. 1/2014 ya DR DAMAS NDUMBARO dhidi ya TFF.
TFF iliwakilishwa na Wakili Msomi Emmanuel Muga na Dr. Ndumbaro
hakufika wala hakuwakilishwa na wakili wake.
Kufuatia kutofika kwa Dk Ndumbaro, Kamati, kwa Azimio moja,
iliamuru TFF itoe wito mpya na mpaka tarehe 14/04/2015 uwe umemfikia Dr.
Ndumbaro, ukimfahamisha tarehe ya kikao kijacho cha kusikiliza rufaa yake.
Lakini taarifa za uhakika za awali ziliyoifikia SALEHJEMBE
kupitia mmoja wa wajumbe wa kamati ya rufaa ya TFF zilionyesha Dk Ndumbaro
hakuwa ameelezwa lolote.
Pia kama ilivyo kawaida ya TFF imekuwa ikitoa taarifa kwa
waandishi siku ya kusikilizwa kwa rufaa mbalimbali, haikufanyika hivyo.
Rufaa hiyo ya Dk Ndumbaro kupinga kufungiwa miaka mitano
ilipangwa isikilizwe kwa siri.
Lakini leo, imeshindikana baada ya baadhi ya waandishi kuanza
kupiga simu wakihoji kuhusiana na rufaa hiyo huku wakitaka kujua kama Dk
Ndumbaro ambaye ni mlalamikaji ana taarifa.
“Tumeona tutaaibika, maana kila mtu ameanza kuuliza. Hii ya
kutaka kusikiliza bila ya kumtaarifu mlalamikaji tumeona itatufanya tuonekane
ni watu wa kubahatisha.
“Tumewataka TFF wampe taarifa ili awepo, hata kama mnamuuma mtu
basi lazima muonyeshe kufuata utaratibu ndigu yangu aaah!” kilieleza chanzo cha
uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment