Mechi ilikuwa tamu, dakika 45 za kwanza zimekamilika huku
wenyeji Yanga wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara imekuwa tamu kutokana na timu zote
kucheza vizuri na kushambuliana kwa zamu.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mliberia, Kpah Sherman na Salum
Telela aliyepiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Haruna Niyonzima.
Bao la Mbeya City limefungwa na mkongwe Themi Felix aliyewatoka
mabeki Nadir Haroub na Oscar Joshua kabla ya kufunga kiufundi kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment