Mechi ya kesho ya Ligi Kuu
England kati ya watani na wapinzani wakubwa Manchester
United dhidi ya Manchester City inaaminika ndiyo ghali zaidi.
Mechi hiyo itapigwa kwenye
Uwanja wa Old Trafford inaaminika ndiyo ghali zaidi katika mji huo, lakini
ghali zaidi katika soka la England.
Timu hizo zinakutana wakati
Man United imetumia kitita cha pauni milioni 278.2 kwa ajili ya usajili wakati Man
City ndani ya misimu mitatu wamemwaga pauni milioni 244.7.
Lakini kwa hali ilivyo,
bado inaonekana timu zote hazina uhakika sana wa kutwaa ubingwa.
Iwapo Man United itamfunga
City, basi itakuwa imemuondoa kwenye mbio za ubingwa wa asilimia 80.
Ushindi kwa Man United pia
utakuwa muhimu kwa kuwa itahitaji kupata moja ya nafasi kati ya nne za juu ili
kushiriki Ligi ya Mabingwa.
Man Unite iko katika nafasi
ya tatu ikiwa na pointi 62 na City
ya nne ikiwa na 61.
Memechi ya kesho itakuwa ni
ya 32 wa kila timu na kila moja itabakiza mechi sita kupigania ubingwa au
kupata nafasi nne za juu.
United imekuwa ikibadilika
na kurejea katika kasi yake huku City ikiporomoka kutoka katika ubora iliokuwa
nao hadi kuonekana inabahatisha kiana.
0 COMMENTS:
Post a Comment