April 12, 2015



MPIRA UMEKWISHAAA
Dk 89, Ngassa tena anaingia eneo la hatari lakini mabeki wanambana vizuri.



Dk 87, Mwagane Yeya anajaribu kuwatoka mabeki wa Yanga lakini Barthez anakuwa mwepesi kuwahi.

Dk 83, Ngassa anaingia vizuri na kushindwa kufunga akiwa hatua chache
Dk 78, Yanga wanaonekana kumiliki mpira zaidi huku Mbeya City wakiwa wanaathirika kutokana na kuwa pungufu.


DK 74, Yanga wanamtoa Sherman, nafasi yake anachukua Mrisho Ngassa
Dk 69, krosi safi ya Joshua, MSuva anapiga kichwa cha kuparaza, kinagonga mwamba na kurejea uwanjani
Dk 61&64, Yanga wanaonekana kutawala zaidi mpira huku wakifika langoni mwa City mara nne na City wanaonekana kujilinda zaidi.

Dk 60, anaingia Salum Telela kuchukua nafasi ya Salum Telela kwa Yanga

Dk 59, Peter Mapunda anaingia kuchukua nafasi ya Deus Kaseke upande wa City

DK 56, Nonga napiga shuti kali, lakini Barthez anadaka kwa mbwembwe kabisa.


KADI NYEKUNDU Dk 53, Themi Felix anapigwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Telela.

Dk 52, kipa Mbeya City anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa faulo wa Niyonzima.


GOOOOO Dk 49, Cannavaro anaunganisha krosi safi ya mpira wa faulo wa Niyonzima na kufunga kwa kichwa safi.

Dk 47, Msuva anapiga shuti akiwa nje kidogo ya lango la Mbeya City, mpira unatoka.


 Dk 46, Yanga wanaanza mashambulizi kwa kasi wakionyesha wamepania kiuongeza bao.

Timu zimekwenda mapumziko Yanga ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1.

Mechi ilikuwa tamu, dakika 45 za kwanza zimekamilika huku wenyeji Yanga wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara imekuwa tamu kutokana na timu zote kucheza vizuri na kushambuliana kwa zamu.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Mliberia, Kpah Sherman na Salum Telela aliyepiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Haruna Niyonzima.

Bao la Mbeya City limefungwa na mkongwe Themi Felix aliyewatoka mabeki Nadir Haroub na Oscar Joshua kabla ya kufunga kiufundi kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic