Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF jana ijumaa ilipokea ugeni
wa makamu wa Rais wa FIFA ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
nchini Jordan, HRH Prince Ali Bin Al Hussein. (picha ya Rais Jamal Malinzi na
HRH Ali imeambatanishwa)
Jioni Prince Ali Bin AliHussein na ujumbe wake walifanya
mazungumzo na Rais wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsinki (Hyatt) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, zaidi waligusia maeneo kadhaa ya
ushirikiano kati ya TFF na Chama cha Mpirwa wa Miguu nchini Jordan (JFA), hasa
katika maeneo ya maendeleo ya mpira wa vijana, makocha na waamuzi.
HRH Prince Ali Bin Al Hussein ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais
FIFA mwaka huu, ameondoka leo mchana kurudi nyumbani kwake Jordan.
0 COMMENTS:
Post a Comment