Licha ya Yanga kuanza kwa sare ya 1-1 nyumbani katika mchezo wao wa awali wa raundi
ya tatu dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia, wachezaji wa kutumainiwa Yanga,
Mrisho Ngassa na Simon Msuva, wametamba kuwa katika mechi ya marudiano
watafanya maajabu na kuwatoa wapinzani wao.
Mchezo
huo wa kuwania kufuzu kuingia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho
ulipigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa na unatarajiwa kurudiwa nchini
Tunisia baada ya wiki mbili zijazo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, wachezaji hao
walisema kwamba wapinzani wao ni wazuri lakini si wa kuwapa nafasi kubwa katika
mechi yao ya pili kwa kuwa kiuwezo ni watu wanaolingana isipokuwa kilichotokea
siku hiyo ni makosa madogo ndiyo yaliwaponza.
“Ni
wazuri lakini si kwamba walituzidi sana, isipokuwa ni makosa ya kimpira
madogomadogo ya uwanjani ndiyo yalisababisha sare, kwa hatua hiyo hatuwezi
kusema kwamba tumetoka, hatuwezi kukata tamaa, huu ni mpira na lolote linaweza
kutokea hata huko kwao, tutakwenda Tunisia kupambana na tutafanya maajabu,”
alisema Ngassa.
Kwa
upande wa Msuva, alisema: “Jamaa siyo wabaya, kiuwezo ni wa kawaida, hauwezi
kusema kama kwa matokeo haya, ndiyo tumetoka, bado tunataka kusonga mbele na
morali hiyo tunayo, tutakwenda kwao kucheza mpira na kuhakikisha tunavuka hapa
tulipo.”
Matokeo
ya sare ya 1-1, yanaiweka Yanga katika mazingira magumu katika mechi ya pili
huku ikitazamiwa kama watapata suluhu watakuwa wametoka, wakitoka 1-1 tena,
hatua ya matuta itaamua na kama ikiwa ni sare ya 2-2 na kuendelea basi itakuwa
neema kwa Yanga.







0 COMMENTS:
Post a Comment