Katika kuhakikisha wanakuwa fiti kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya Mgambo JKT, kiungo
mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okiwi na beki wa pembeni, Hassani Kessy,
wametengwa na kupewa mazoezi maalum.
Simba inatarajiwa
kuvaana na Mgambo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katika mechi
ya Ligi Kuu Bara.
Hiyo yote ni
katika kuwaweka fiti wachezaji hao tegemeo wenye kasi baada ya kuikosa mechi
iliyopita dhidi ya Mbeya City kwa matatizo tofauti, mchezo ambao ulimalizika
kwa Simba kufungwa mabao 2-0.
Okwi aliikosa
mechi ya Mbeya City kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano huku Kessy yeye
akiwa na matatizo na uongozi baada ya kugomea mazoezi ya timu hiyo akidai
kumaliziwa fedha yake ya usajili na nyumba ya kulala.
Wachezaji hao,
wakiwa chini ya kocha msaidizi, Selemani Matola, walipewa mazoezi ya kukimbia
mbio fupi na ndefu kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kocha
mkuu wa timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic kupendekeza.
Wachezaji hao,
walitumia kama dakika 15 kufanya programu hiyo maalum kuanzia saa 10:30 hadi 11:15
kabla ya kutakiwa kunywa maji na kupumzika.
Chanzo makini
kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa kocha huyo anafanya hivyo ili kuhakikisha
wachezaji hao wanacheza leo kwa kuwa ni mechi muhimu.







0 COMMENTS:
Post a Comment