Katika kuhakikisha kikosi cha Coastal Union kinakuwa bora na cha
ushindani msimu ujao, kamati ya usajili wa timu hiyo imejipanga kusajili
wachezaji wenye uwezo kulingana na mahitaji huku wachezaji wote wa kigeni
wakifunguliwa milango ya kuondoka kutokana na wote kumaliza mikataba yao.
Coastal ina wachezaji wanne wa kigeni ambao ni mshambuliaji Rama
Salim (Kenya), Ike Bright Obina (Nigeria), Lutimba Yayo (Uganda) na Itubu Imbem
(DR Congo) ambao wote mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu.
Kiongozi wa kamati ya usajili wa timu hiyo, Salim Bawazir, amesema
msimu ujao watakuwa makini kwenye suala ya usajili.
“Wachezaji wengi wanamaliza mikataba yao lakini kwa upande wa
maprofesheno, nao wote wanamaliza mikataba, ambaye atakuwa tayari kubaki hakuna
shida lakini ni ruksa hata kuondoka.
“Malengo yetu ni kuwabakiza wachezaji wengi wenye msaada kwenye
timu,” alisema Bawazir.








0 COMMENTS:
Post a Comment