Mshambuliaji tegemeo
wa Yanga, Amissi Tambwe amesema Yanga ia nafasi ya kushinda mechi yake ya
ugenini ya Kombe la Shirikisho dhidi ya FC Platinum.
Yanga inaondoka
nchini kesho kwenda Zimbabwe kuwafuata FC Plutnum katika mechi ya pili baada ya
kuwa imeshinda kwa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza jijini Dar.
“Mechi itakuwa ngumu
kama hapa nyumbani, kwani katika soka wakati mwingine nyumbani na ugenini
hakuna tofauti.
“Kikubwa ni sisi
kujituma na kufanya vizuri, kocha anajua tunahitaji nini na sisi tunajua
tumeelekezwa nini,” alisema tambwe.
“Tuna kikosi kizuri,
ninawaamini wenzangu na kama tukitulia, naamini tunaweza kushinda hata ugenini.”
Tambwe ni kati ya
waliofunga katika ushindi huo dhidi ya Platinums jijini Dar.







0 COMMENTS:
Post a Comment