| YANGA WAKISHANGILIA BAO BAADA YA NAHODHA CANNAVARO KUFUNGA BAO... |
Ligi Kuu Bara inatarajia
kuendelea kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati vinara wa
ligi hiyo Yanga watawakaribisha timu ya Stand United kutoka mjini Shinyanga.
Yanga inaonekana kuwa na
hasira baada ya kupata sare katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya
Etoile du Sahel.
Kesho itakuwa na kazi
kubwa ya kurudisha imani ya mashabiki wake na lazima ionyeshe kiwango ili
kuamsha matumaini kwamba itafanya vema katika mechi ijayo dhidi ya Waarabu huko
nchini Tunisia.
Stand nao wametamba
kwamba hawako nalenale na wanataka kupambana na kushinda mechi hiyo kuwa na
uhakika zaidi wa kubaki Ligi Kuu Bara.
Si lahisi kwa kila upande
lakini Yanga lazima ishinde ili kujiweka sawa kwa kuwa tofauti ya pointi kati
yake na Azam FC ni nne tu na Yanga ina mchezo mmoja mkononi kwa kuwa Aam FC
imeshuka dimbani mara 22 na yenyewe 21.







0 COMMENTS:
Post a Comment