April 26, 2015



Uongozi wa klabu ya Yanga unapenda kuwaalika wananchi wa Tanzania na nchi jirani kuungana Basi kesho katika shamrashamra za ushindi wa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu Bara.


Katibu Mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha amesema wao kama uongozi tayari wameanza maandalizi ya kusherehekea ubingwa Kwa staili ya tofauti kabisa ambayo wataitumia katika mchezo wao wa kesho  dhidi ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Sisi kama Yanga tumejipanga Kwa staili tofauti Kabisa katika kuuchukua ubingwa wa ligi kuu na napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha mamia na maelfu ya Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini kuja kuungana na sisi katika surprise ya kuchukua ubingwa kesho."

Awali akizungumzia safari ndefu ya kuusaka ubingwa Dk Tiboroha amesema wametoka Mbali kimafanikio Kwa kuweza kushinda Michezo Mingi na kilichobaki kesho ni kitu kitu kidogo Sana kwao kumaliza safari Ndefu Ya kuusaka ubingwa.

"Hatuwezi kula ng'ombe mzima kisha tushindwe kumaliza mkia ambao sisi tutaula kama supu," aliongeza Tiboroha.

Kwa upande wake Mkuu wa ufarahiee ya Habari na Mawasiliano Ya Yanga, Jerry Muro amesema tayari wanachama na viongozi wa Yanga kutoka maeneo mbalimbali nchini wameanza kuwasili jijini Kwa ajili Ya kushuhudia mchezo wa kesho ambao kwao wameamua kuutoa Kama Zawadi Ya maadhimisho Ya Miaka 52 Ya muungano wa Tanzania na Zanzibar.

"Kwa Mara Ya kwanza Kabisa tunataka kuchukua ubingwa Kwa style ya tofauti Kabisa hivyo natoa wito Kwa wananchi na haswa mashabiki na wanachama wa Yanga popote pale walipo waungane nasi kesho kwenye shamrashamra za ubingwa.
"

Imetolewa na idea ya Habari na Mawasiliano Yanga-Makao Makuu

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic