Etoile du Sahel wamefanya
kikao kizito kuhakikisha wanaing’oa Yanga.
Kikao hicho kimejumuisha
wachezaji wakongwe wa zamani wa timu hiyo, wakuu wa makundi ya mashabiki pamoja
na viongozi wa zamani.
Kikao hicho kimefanyika
makao makuu ya klabu hiyo mjini Sousse, Tunisia na imeelezwa hoja nyingine
ilikuwa ni kujadili suala la Ligi Kuu ya Tunisia pamoja na masuala mengi ya
uchaguzi.
Ingawa mengi
yaliyozungumziwa yamefanywa ni siri na kutajwa machache, imeelezwa Yanga
ilikuwa ni sehemu ya ajenda kuu.
Baadhi ya wajumbe walionya
Etoile kuhakikisha hawaidharau Yanga hata kidogo na ikiwezekana wajiandaa
utafikiri walipoteza mechi jijini Dar.
Yanga na Etoile zilitoka
sare ya bao 1-1 jijini Dar, hivyo Yanga inatakiwa kushinda au sare ya kuanzia
bao 2-2 ili isonge mbele katika mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho.
Kwa Mungu yote yanawezekana.
ReplyDelete