Baada
ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na kupata timu tatu
zitakazouwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya mabingwa ya mikoa ya TFF sasa
ni fainali ya bingwa wa jumla kwenye Uwanja wa Karume jijini, kesho.
Timu
zinazokutana kesho katika fainali hiyo ni Zakhem FC dhidi ya FFU SC ambazo
zitashuka dimbani majira ya Saa 10 Jioni.
Kwa
mujibu wa kamati ya mashindano ya Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), timu
zilizofanikiwa kuuwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya maabingwa ni pamoja
na Zakhem FC, FFU SC na Changanyikeni SC.
Mwenyekiti
wa DRFA, Almas Kasongo,ameipongeza kamati hiyo ya mashindano kwa kusimamia
vizuri uendeshaji wa ligi tangu ilipoanza.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA
DRFA, OMARY KATANGA.
0 COMMENTS:
Post a Comment