Kama si juhudu za wachezaji wa Bayern Munich
basi mshambuliaji Robert Lewandowski na beki Jerome Boateng wangeishia pabaya.
Wawili hao walitaka kuzichapa katika mazoezi ya
timu hiyo jana baada ya Lewandowski kumuangusha Boateng wakati wakigombea
mpira.
Kitendo hicho kilionyesha kumuudhi beki huyo
mwenye asili ya Ghana na kusababisha ugomvi huo huku wakitaka kuzichapa
kavukabu, lakini lakini juhudi za wachezaji pamoja na maneno ya kocha Pep
Guardiola yalisaidia wachezaji hao kusitisha zoezi kao la kutaka kuchapana.
0 COMMENTS:
Post a Comment