Kinda la Kibrazil, Nathan ametua Chelsea na
kumwaga wino kwa pauni milioni 4.5.
Kijana huyo aliyekuwa nyota katika kikosi cha
Brazil chini ya miaka 19, amesaini mkataba wa kuichezea Chelsea jana Jumatatu.
Baada ya hapo akatupia kwenye mtandao wa kijamii
akiwa anasaini na baadaye akipiga picha katika makao makuu ya klabu hiyo jijini
London.
Kijana huyo amekuwa gumzo sana kutokana na uwezo
wake mkubwa na timu kadhaa zilikuwa zikimuwania kabla ya Chelsea kumnasa.
Hata hivyo, bado Chelsea haijatoa taarifa rasmi
kuhusiana na kumnasa Nathan.
0 COMMENTS:
Post a Comment