Mwaka wa neema Jangwani! Wakati wakiwa kwenye shangwe za ubingwa,
wachezaji wa Yanga wamezidi kupata ‘madili’ nje ya nchi, ambapo Simon Msuva,
Mrisho Ngassa wanahitajika Afrika Kusini huku straika Dan Mrwanda akipata ofa
nchini Thailand.
Mtu wa karibu na nyota huyo amesema kuwa, Mrwanda anataka kuwaandikia
barua Yanga akitaka aachwe punde tu baada ya ligi kumalizika ili awahi dirisha
la usajili nchini humo.
Chanzo hicho kimesema iwapo viongozi watamgomea kutokana na kuwa na
mkataba, atakubali yaishe lakini ndoto yake ni kusaka changamoto kwingine.
Alisaini mwaka mmoja akitokea Polisi Moro.
“Kuna timu moja nchini Thailand inamtaka na anasema ni lazima aende,
lakini yote itatokana na baraka za viongozi wa Yanga. Baada ya ligi amepanga
kuwaandikia barua ya kuomba aachwe ili awahi usajili ambao kwao unapishana na
Tanzania,” alisema rafiki huyo.
Alipoulizwa Mrwanda, alisema: “Ni mapema sana, tungoje ligi iishe
mengine yatafuata baadaye.”







0 COMMENTS:
Post a Comment