Beki kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, yupo nje ya kikosi cha Yanga kutokana na
kusumbuliwa na malaria lakini ameweka mipango yake ya kusafiri akipitia Kenya
kuzungumza na Gor Mahia juu ya masuala ya usajili kisha kwenda kwa Waarabu wa
El Merreikh.
Twite ameliambia gazeti hili kuwa, akitokea Kenya ataenda DR Congo kumuona mama
yake anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo kisha ataonana na viongozi wa El
Merreikh ya Sudan.
“Malaria inanisumbua ndiyo maana nipo nje ya uwanja lakini
nitaondoka muda wowote ndani ya siku mbili hizi kwenda nyumbani kumuona mama nikipitia
Kenya.
“Nahitaji kuzungumza na viongozi wa Gor Mahia, walishanipigia simu
tukaelewana, nikifika huko tutazungumza zaidi,” alisema Twite na kuongeza:
“Nikimalizana na Gor Mahia nitakutana na Merreikh nikiwa Congo,
nilizungumza nao kuwa nikienda Congo tutakutana tuzungumze.”







0 COMMENTS:
Post a Comment