Baada ya kikosi cha Simba kushindwa kupata tiketi ya kushiriki
michuano ya kimataifa kwa msimu wa tatu mfululizo, kocha na mchezaji wa zamani
wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ni aibu kwa klabu kubwa kushindwa
kushiriki kimataifa.
Julio amesema kuwa viongozi na wachezaji wameshindwa kuitendea haki
klabu hiyo na badala yake wanaangalia zaidi maslahi binafsi.
“Hawaitendei haki Simba ile ambayo mimi naifahamu tangu enzi hizo, hii ni kutokana na aina
ya viongozi waliopo pamoja na wachezaji kuendekeza starehe.
“Kitu kingine ni kubadili makocha kila kukicha, hicho nacho
kimesababisha wapoteze mwelekeo. Wanatakiwa kujipanga upya wasajili wachezaji wenye uwezo,” alisema
Julio.
Simba inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Bara na haitaweza
kushiriki kimataifa, nafasi ambayo imetua kwa Yanga na Azam.







0 COMMENTS:
Post a Comment